Kupambana na ujinga… kituo cha Tunasoma ili tuishi kimekamilisha mitihani ya hatua ya pili

Kituo cha (Tunasoma ili tuishi) chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu kimehitimisha mitihani ya hatua ya pili kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Sayyid Swalahu Mahadi amesema “Mitihani ya hatua ya pili imewahusu wale waliokosa nafasi ya kusoma katika umri mdogo, wamefanya mtihani wa kusoma, kuandika, hesabu na utamaduni”.

Akaongeza kuwa “Semina imepata muitikio mkubwa wa watu wenye umri tofauti, imedumu kwa muda wa miezi mitano, walikua wanasoma siku tatu kwa wiki”.

Akaendelea kusema “Lengo la semina hizi ni kuwafundisha washiriki kusoma na kuandika pamoja na mambo mengine muhimu katika Maisha yao, sambamba na kuhimiza usomaji wa Qur’ani tukufu na ziara za Maimamu watakatifu (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: