Imetoa walimu wengi.. Maelezo kuhusu masomo ya hauza katika shule ya Daarul-Ilmi

Shule ya Daarul-Ilmi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imetoa maelezo kuhusu masomo ya hauza, ikabainisha kuwa walimu wengi wamehitimu katika shule hiyo.

Mkuu wa shule Sayyid Haidari Karbalai amesema, Hakika mji mtukufu wa Karbala na Najafu ndio kitovu cha elimu ya Ahlulbait (a.s) na sehemehu sahihi ya mtu kuja kusoma”.

Akaongeza kuwa “Masomo ya hauza yamegawanyika sehemu tatu ambazo ni: (Muqadimaat, Sutuuh na Bahthul-Khaarij)”. Akafafanua kuwa, “Muqadimaat inahusisha masome na mada nyingi, Sutuuh masomo yanapungua na Bahthul-Khaarij ni kiwango cha kuelekea katika Ijtihadi”.

Akaendelea kusema “Wamehitimu walimu wengi wa masomo ya Itikadi na Fiqhi Pamoja na masomo ya sheria na utambuzi wa Rasaailu (vitabu) vya Fiqhi”.

Kuhusu malengo la shule ya Daarul-Ilmi amesema kuwa “Hauza inalenga kukuza elimu ya Dini na kulinda misingi ya Dini na madhehebu”.

Mwezi ujao tutafungua kituo cha masomoya ya Aqida kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa shule.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: