Kitengo cha Dini kimeswali swala ya Ayaat ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeswali swala ya Ayaat ndani ya ukumbi wa malalo tukufu baada ya Adhuhuri ya leo siku ya Jumanne.

Imamu wa swala hiyo alikua Shekhe Swalahu Karbalai, haram tukufu imejaa watu waliokuja kuswali swala hiyo ya wajibu, huku wakishuhudia tukio adimu la kupatwa kwa jua.

Swala hilo ilihitimishwa kwa kusoma Duaau-Faraj ya Imamu Mahadi msubiriwa (a.f), na kumuomba Mwenyezi Mungu awalinde Maraajii wetu wakuu na alilinde taifa letu tukufu.

Mji wa Karbala na miji mingine ya Iraq, imeshuhudia kupatwa kwa jua kulikoanza saa saba mchana na kukaendelea kwa muda wa saa mbili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: