Kamati ya wizarani inayohusika na viwango vya elimu chini ya wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu imefanya mahojiano na watumishi wa chio kikuu cha Al-Ameed kwa njia ya mtandao.
Mahojiano hayo yamefanywa kwa kutumia mtandao wa (zoom), chini ya ushiriki wa rais wa chuo Dokta Muayyad Imraan Ghazali, Dokta Maitham Saidi, Dokta Alaa Mussawi Pamoja na wakuu wa vitengo na wasaidizi wao.
Ghazali ameanza kwa kuwakaribisha wajumbe kutoka wizarani, kisha akafuata itifaki ya uendeshaji wa kikao hicho.
Likapitiwa jina la mshiriki mmoja mmoja kwa kuhakikiwa na majina yaliyopelekwa wizarani, kisha wakaanza kujadiliana.