Atabatu Abbasiyya imezawadia watuishi wake waliotengeneza dirisha jipya la malalo ya bibi Zainabu (a.s) na wale waliolisafirisha hadi kwenye haram yake takatifu nchini Sirya.
Hafla ya utoaji wa zawadi imehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, viongozi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, mkuu wa mkoa wa Karbala Mhandisi Naswifu Jaasim Alkhatwabi na watumishi wa kitengo cha kutengeneza madirisha ya makaburi na milango mitukufu.
Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyo somwa na Sayyid Haidari Jalukhani Mussawi, ikafuatiwa na ujumbe kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria, akasisitiza kauli ya bibi Zainabu (a.s) aliyotoa mbele ya muovu isemayo “Fanya vitimbi vyako na njama zako..”.
Naye katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini akasema “Dirisha limetengenezwa na kusafirishwa na raia wa Iraq tena watumishi wa Ataba tukufu, Abulfadhil Abbasi (a.s) ameonyesha matunda yake Sham kwa kupeleka zawadi kubwa ambayo ni dirisha hilo tukufu”.
Akaongeza kuwa “Dirisha hilo zi zawadi kubwa iliyowekwa juu ya malalo takatifu ya bibi Zainabu (a.s), leo Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya usimamizi wa kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi inawapa zawadi watu wote walioshiriki kutengeneza dirisha hilo na kuliweka kwenye malalo takatifu huko Sirya”.
Mkuu wa mkoa wa Karbala Mhandisi Naswifu Jaasim Alkhatwabi akasema “Kiwanda cha kutengeneza madirisha ya makaburi cha Atabatu Abbasiyya tukufu kinatengeneza madirisha mazuri, yatupasa kujivunia” akaongeza kuwa “Utengenezaji wa dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s) unaonyesha kiwango cha juu kabisa cha mapenzi kwa Ahlulbait (a.s)”.
Hafla ikahitimishwa kwa kugawa zawadi kwa mafundi waliotengeneza dirisha tukufu la malalo ya bibi Zainabu (a.s), kikosi cha waandishi wa Habari waliokuwa wakitangaza Habari hiyo na askari kutoka kikosi cha Abbasi cha wapiganaji, waliosimamia usafirishaji wa dirisha hilo.