Mjumbe wa kamati kuu ya uongozi katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Liith Mussawi, amehimiza umuhimu wa kuchunga muda wa kazi na kuutumia vizuri katika kuhudumia malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na mazuwaru wake.
Sayyid Mussawi ameyasema hayo kwenye kikao cha viongozi na watumishi wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, “hakika kazi tukufu ya kuhudumia malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ni neema kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu inayofaa kushukuriwa”.
Akaongeza kuwa “Tunatakiwa kuchunga muda wa kazi na kuutumia vizuri, kwa kufanya hivyo tutakuwa na mafanikio makubwa katika kuhudumia malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na mazuwaru wake watukufu”.
Akasisitiza umuhimu wa kuzingatia maelekezo ya idara chini ya uongozi mkuu wa Ataba tukufu.
Kikao hicho ni sehemu ya mfululizo wa vikao-kazi vinavyo fanywa kujadili utendaji na mafanikio.