Kitengo cha Dini kinaendelea kutoa semina za mtumishi bora

Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia idara ya Tablighi kinatoa semina za (Mtumishi bora) kwa wahudumu wa Abulfadhil Abbasi (a.s).

Mkufunzi wa semina hiyo Sayyid Mudhwaharu Husseini amesema “Semina inatolewa na idara ya Tablighi kwa wahudumu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, inalenga kuwajenga kimaadili, kifiqhi na kiimani”.

Akaongeza kuwa “Semina hii imedumu kwa muda wa siku (15), ilikua na mada tatu, Akhlaq, Fiqhi na Aqida, kila mada imefundishwa siku tano”.

Tambua kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya semina mbalimbali zinazo lenga kuwajenga wahudumu wake kimaadili, kielimu na kitamaduni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: