Maahadi ya Qur’ani tukufu imefanya hafla ya wanafunzi miamoja waliohitimu

Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya imefanya hafla ya wahitimu miamoja wa semina za kanuni za usomaji wa Qur’ani tukufu.

Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Aljaburi amesema “Hawa ni wahitimu wa semina saba za kanuni za usomaji wa Qur’ani tukufu zilizo fanya Maahadi na kwenye baadhi ya vituo vilivyo chini yake, baada ya semina hizo wamefanya mitihani na kufaulu, sasa wako tayali kuingia katika semina za kuhifadhi msahafu mtukufu”.

Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu kisha ikasomwa kaswida iliyo eleza utukufu wa Qur’ani na msomaji wake, yakafuata maswali kuhusu Qur’ani, kisha ugawaji wa zawadi, halafu wanafunzi wakafanya igizo kuhusu baadhi ya changamoto za familia anazopata mtu aliyetelekeza Qur’ani, hafla ikahitimishwa kwa kugawa vyeti kwa wahitimu, na kusoma Duaau-Faraj ya Imamu wa zama (a.s) kwa mujibu wa maelezo ya Aljaburi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: