Kitengo cha Dini: Lengo letu ni kufikisha hukumu za kisheria kwa mazuwaru

Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimesema kuwa lengo lake ni kufikisha hukumu za kisheria kwa mazuwaru.

Makamo rais wa kitengo hicho Shekhe Aadil Wakili amekiambia kituo cha Habari kuwa “Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinamajukumu mengi, miongoni mwa majukumu hayo ni kufafanua hukumu za kisheria na kujibu maswali”.

Akaongeza kuwa “Tunapokea maswali mengi yanayohitaji majibu ya kisheria Pamoja na maombi ya vitabu vidogo vidogo kama vile (Je! Unajua) na vitabu vingine, kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi vitavu hivyo hutolewa bure kwa mazuwaru kupitia dirisha la maktaba ya nje”.

Kuhusu malengo ya kitengo amesema kuwa “Malengo ya kitengo cha Dini hufikiwa kwa kueleza hukumu za kisheria kwa mazuwaru kupitia mimbari za ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi kwa kutoa mawaidha ya kila siku na usomaji wa Qur’ani”.

Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinafanya majukumu yake kila siku kwa kujibu maswali na kubainisha hukumu za kisheria Pamoja na kusahihisha usomaji wa Qur’ani kwa mujibu wa maelezo ya Wakili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: