Katika awamu ya 46.. Atabatu Abbasiyya inashiriki kwenye maonyesho ya kimataifa jijini Bagdad

Katika awamu ya 46 Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki kwenye maonyesho ya kimataifa jijini Bagdad yanayofanywa chini ya kauli mbiu isemayo (tamaduni na changamoto ya maendeleo ya dunia).

Kiongozi wa idara ya Habari katika shirika la Alkafeel Sayyid Mustafa Ni’mah Muhammad amesema kuwa “Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia mashirika yake imekua ikishiriki kwenye matukio ya kimataifa na kitaifa, ikiwa ni pamoja na maonyesho ya kimataifa ambayo hufanywa jijini Bagdad”.

Akaongeza kuwa “Ushiriki wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye maonyesho ya kimataifa yanayofanyika Bagdad haujaishia kwenye shirika la Khairul-Juud na Nurul-Kafeel peke yake, bali kunaushiriki wa kitengo cha miradi ya kihandisi, Idara ya maji, idara ya vifaa vya ujenzi. bila kusahau kituo cha Habari Alkafeel, Darul-Kafeel ya uchapishaji na usambazaji”.

Akaendelea kusema “Shirika la uchumi Alkafeel limeshiriki kwenye maonyesho ya Bagdad ya arubaini ya sita likiwa na bidhaa za kilimo, wanyama, asali na maji ya Alkafeel”.

Akabainisha kuwa “Lengo la ushiriki huo ni kuonyesha picha halisi ya uwezo wa Atabatu Abbasiyya kwenye sekta tofauti, viwanda, ujenzi na kilimo, jumla ya nchi 12 zimeshiriki kwenye maonyesho haya na mashirika ziadi ya 350 ya kimataifa na kitaifa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: