Kitengo cha uhusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimepokea vijana (50) kutoka mkoa wa Barsa.
Kiongozi wa idara ya mawasiliano Sayyid Rasuli Twaiy amesema kuwa “Tumepokea kundi la vijana kutoka Basra kufuatia mawasiliano tuliyofanya na muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika mji wa Basra Shekhe Jasim Swimiri, tumewapa nafasi ya kuuliza maswali baada ya mhadhara uliotolewa na Mheshimiwa Sayyid Muhammad Amidi kiongozi kutoka ofisi ya muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu”.
Kitengo cha mahusiano hupokea wageni kutoka maeneo tofauti na kuwapa sehemu muwafaka za malazi, sambamba na kuwaandalia ratiba maalum na kuwapeleka sehemu mbalimbali ndani na nje ya mji wa Karbala. Akasema kuwa “Jukumu la kuwasafirisha kutoka mkoani kwao hadi Karbala na kuwarudisha linafanywa na kitengo cha utalii wa kidini cha Ataba tukufu”.