Kuanza shindano la Qur’ani tukufu la kitaifa awamu ya tatu

Kitoa cha kitaifa cha maarifa ya Qur’ani kwa kushirikiana na kituo cha miradi ya Qur’ani katika Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya kinafanya shindano la Qur’ani la kitaifa awamu ya tatu.

Mkuu wa kituo cha miradi ya Qur’ani Sayyid Hasanain Halo amesema “Shindano limeanza siku ya Ijumaa ndani ya jengo la Alqami katika mji mtukufu wa Karbala”.

Naye msimamizi wa shindano hilo Sayyid Ali Abdusataar Alkhafaji amekipongeza kituo cha miradi ya Qur’ani kwa kazi kubwa ya kufundisha vijana na kuwaendeleza katika sekta ya Qur’ani, sambamba na kuwajengea moyo wa ushindani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: