Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Mustafa Murtadha Aaludhiyaau-Dini amepongeza Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu kitengo cha uandishi kwa kukamilisha uchapishaji wa msahafu ulioandikwa na mazuwaru wa Arubainiyya.
Mheshimiwa katibu mkuu amekagua nakala ya msahafu huo mbele ya rais wa Majmaa-Ilmi Dokta Mushtaqu Ali na baadhi ya watumishi.
Huu ni msahafu wa kwanza kuandikwa kwa njia hii, haijawahi kutokea mazuwaru wa bwana wa mashahidi kuandika msahafu, kumbuka msahafu huu umeandikwa wakati wa ziara ya Arubainiyya mwaka 1444h.
Jumla ya mazuwaru (1750) kutoka nchi (16) wameshiriki kuandika msahafu huo.
Rais wa Majmaa-Ilmi Dokta Mustaqu Ali amesema “Kutokana na kufanyia kazi mtazamo wa kusambaza utamaduni wa kusoma Qur’ani katika jamii, na mtazamo wa kimkakati tulionao katika Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu, tuliamua kuanza harakati ya kuandika msahafu mtukufu kwa mikono ya mazuwaru wa ziara ya Arubainiyya”.
Akaongeza kuwa “Msahafu huu umetolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu, umeandikwa na mazuwaru kwa lengo la kuweka mazingira ya kiroho zaidi na kielimu, kwani mazuwaru wanaokuja Karbala wanautukufu mkubwa”.