Ugeni kutoka muungano wa wasoma Qur’ani katika mkoa wa Waasit umepongeza mradi wa Arshu-Tilawah unaofanywa kila wiki

Kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, kimepokea ugeni kutoka muungano wa wasoma Qur’ani katika mkoa wa Waasit, uliohudhuria kwenye kikao cha usomaji wa Qur’ani ndani ya haram tukufu ya Abbasi.

Ugeni huo umepongeza kituo cha miradi ya Qur’ani, ikiwa ni pamoja na uendeshaji wa mradi wa Arshu-Tilawah unaofanywa kila wiki ndani ya ukumbi wa Nuru-Abbasi uliopo ndani ya haram takatifu.

Wageni wameshiriki kwenye hafla ya usomaji wa Qur’ani iliyofanywa ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kama sehemu ya kukumbuka kifo cha Fatuma Zaharaa (a.s).

Vikao vya usomaji wa Qur’ani katika mradi wa Arshu-Tilawa hurushwa moja kwa moja na chanel ya Qur’ani tukufu katika luninga ya Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: