Katika tafsiri ya Shekhe Muhammad Jawadi Albalaghi “Toleo jipya”

Hivi karibuni Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya kupitia Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu imetoa kitabu cha (Tafsiri ya Shekhe Muhammad Jawadi Albalaghi -r.a-).

Kitabu hicho kinaangazia mambo muhimu katika masomo ya maarifa pamoja na kufungua mlango wa kujadili kielimu mafanikio ya wanachuoni wetu.

Kitabu cha (Tafsiri ya Shekhe Muhammad Jawadi Albalaghi) kinafungua pazia ya kuangazia wanachuoni wa kiislamu na mchango wao wa kielimu katika historia ya elimu, hakika ni wanachuoni waliofungua milango ya elimu kwa waislamu na kuwaongoza kwenye njia ya uongofu na elimu, naye ni mmoja wa wafarisi wa kishia mwenye athari katika maktaba za waislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: