Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi ametembelea kitivo cha udaktari wa binaadamu katika chuo kikuu cha Alkafeel mjini Najafu.
Mheshimiwa Sayyid Swafi amehimiza umuhimu wa vifaa vyote vya lazima vitakavyo kiwezesha kitivo hicho kuwa cha kimataifa, na kufikia lengo la Ataba tukufu la kutoa huduma bora kwa jamii.
Kitivo hicho kimepata kibali rasmi kutoka wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu, baada ya kukamilisha vigezo vyote vinavyo hitajika, ikiwa ni pamoja na majengo, kumbi za madarasa, vifaa vya kufundishia, maabara sambamba na kuwepo kwa hospitali maalum itakayo tumika kwa masomo ya vitendo kwa madaktari, aidha chuo kimeajiri walimu mahiri wenye uzowefu na weledi mkubwa.
Kitivo hicho kimeanza kupokea wanafunzi wa mwaka wa masomo (2022 – 2023), na kinatoa wito wa kila anayetaka kujiunga na chuo hicho aombe kwa njia ya mtandao.