Kongamano la kielimu Al-Ameed.. wageni kutoka nje ya Iraq wasisitiza kuwa la kimataifa

Dokta Rola Yaziji muwakilishi wa wageni kutoka nje ya Iraq katika kongamano la kielimu Al-Ameed linalofanywa kwa mwaka wa sita amesisitiza ujumuishi wa mada za kongamano na umataifa wa kongamano hilo.

Kongamano linafanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) katika Atabatu Abbasiyya, chini ya anuani isemayo (Palagrafu za Habari zisizofaa -kinga na changamoto-) tarehe (10-11/Novemba/2022) sawa na tarehe (15-16 Rabiu thani 1444h).

Yaziji amesema kuwa “Leo tunaangalia maudhui tanzu katika dunia ya sasa, uwepo kwa washiriki wa kongamano kutoka nje ya Iraq kunamaanisha umataifa wa kongamano hili na umuhimu wake”.

Akaongeza kusema mtafiti huyo kutoka kilebanoni “Leo tumekuja kubadilishana fikra na kujadili mambo kielimu yatakayo tusaidia kupata ukweli na kuutangaza kwenye vyombo vya Habari”.

Kongamano limepambwa na watafiti wengi kutoka ndani na nje ya Iraq, litakuwa na vikao vitatu, jumla ya mada (17) zitawasilishwa kwenye vikao hivyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: