Kuendelea kwa vikao vya kitafiti katika kongamano la Al-Ameed awamu ya sita

Baada ya Adhuhuri ya siku ya Alkhamisi katika Atabatu Abbasiyya, vimeanza vikao vya kitafiti katika kongamano la Al-Ameed awamu ya sita.

Katika kikao hicho jumla ya mada saba zimewasilishwa:

  1. Khutuba za ugombanishi katika zama za bani Abbasi, Dkt Imaad Jaghim Awidi.
  2. Athari ya vyombo vya Habari kutokana na Qur’ani tukufu na khutuba za Imamu Hussein (a.s), Dkt Amaar Hassan Abduzahra.
  3. Propaganda za vyombo vya Habari na mchango wake katika kupotosha jamii.. tafiti katika muongozo wa Qur’ani tukufu na sunna za Mtume, Dkt. Amru Zuhair Ali.
  4. Upotoshaji wa vyombo vya Habari kuhusu historia ya Imamu Hassan na Hussein (a.s) uliofanywa na utawala wa Umawiyya mwaka (41 – 64h), Dkt. Salami Jabaar Munshid A’aajibi/ mtafiti Zainabu Nadhim Koni.
  5. Mifumo ya kiarabu katika vyombo vya Habari, Dkt. Sahar Naji Fadhili.
  6. Turathi za mifumo ya kiarabu katika kujibu Habari za kifalme, Dkt. Twaha Hussein Issa.
  7. Kupotosha mafundisho ya Dini katika khutuba za vyombo vya Habari vya bani Abbasi, Dkt. Ali Ismaili Khaliil.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: