Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya inatoa mhadhara wa kwanza kuhusu Qur’ani kwenye mradi maalum wa vyuo vikuu na Maahadi.
Mradi huu unasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tawi la Baabil chini ya Majmaa-Ilmi.
Mhadhara wa kwanza umetolewa mbele ya wanafunzi wa masomo ya Qur’ani katika chuo kikuu cha kiislamu tawi la Baabil chini ya walimu bobezi na wanaokubalika na Maahadi pamoja na chuo kikuu.
Kamati inayosimamia mradi huo, imesisitiza umuhimu wa kujifunza elimu za Qur’ani kwa nadhariyya na vitendo, kwani kufanya vivyo ni kutengeneza kizazi cha watu wanaojitambua na wenye kushikamana na Qur’ani tukufu.
Majmaa-Ilmi imeandaa ratiba maalum inayojumuisha miradi tofauti ya Qur’ani tukufu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na Maahadi itakayotekelezwa mwaka huu wa masomo.