Mkuu wa ofisi ya Mheshimiwa kiongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya Dokta Afdhalu Shami amepokea ugeni kutoka chama cha wafungwa wa kisiasa na familia na mashahidi kutoka wilaya ya Nu’maniyya mkoani Waasit.
Kiongozi wa chama hicho Dokta Fadhil Alkhuzai amesema “Miongoni mwa harakati za chama chetu ni kutembelea Ataba mbili tukufu katika mji wa Karbala na kukutana na viongozi wa Ataba hizo kwa ajili ya kufikisha salamu za wafungwa na familia za mashahidi wa Waasit”.
Akaongeza kuwa “Katika kikao chetu na Dokta Afdhalu Shami tumeeleza changamoto zetu za kiutendaji ikiwa ni pamoja na ugumu wa kuendesha kesi na kupatikana kwa haki za mashahidi, mambo ambayo ufuatiliaji wake huchukua muda mrefu na kuwa sababu ya kupoteza haki”.
Ugeni umewasilisha maombi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ombi la kujenga hospitali katika wilaya ya Nu’maniyya itakayo rahisisha kutoa huduma kwa watoto wa mashahidi na wafungwa wa kisiasa.