Kitengo cha utumishi kimesema: Tunasehemu maalum zenye viti-mwendo vya watoto na wazee na hupewa kwa urahisi

Wahudumu wa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya husaidia mazuwaru watoto na wazee kwa kuwapa viti-mwendo na kuwapeleka kufanya ziara kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Makamo rais wa kitengo Sayyid Muhammad Harbi amesema: “Tuna sehemu nyingi ambazo tumeweka viti mwendo maalum kwa watoto na wazee wenye mahitaji maalum, ambapo huwapa viti mwendo pamoja na watumishi ambao huwashindikiza kwenda kufanya ziara, pale inapokua ni vigumu kufanya wenyewe bila msaada”.

Kuhusu namna ya kupata kiti-mwendo amesema kuwa “Mtu hupewa kitimwendo baada ya kupata kibali maalum”, akasema “Idara inaviti-mwendo kati ya 250 – 300 vilivyo wekwa sehemu tofauti ikiwa ni pamoja na neo la karibu na haram tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: