Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu imetoa link ya kujisajili kwenye semina za Qur’ani

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imetoa link ya kujisajili kwenye semina za Qur’ani zinazofanywa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na Maahadi katika mji wa Najafu.

Wasimamizi wa semina hizo ni Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu chini ya Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya kwa kushirikiana na vyuo vikuu na Maahadi zilizopo mkoani.

Katika semina hizo wanafundishwa usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu na kanuni za usomaji wa Qur’ani, aidha kuna mashindano yanayoendeshwa kwa njia ya mtandao, nadwa na maonyesho ya Qur’ani na mambo mengine ya kidini.

Kwa maelezo zaidi piga simu namba: 07722990777.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: