Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu hudumisha usafi kwenye uwanja huo mtakatifu

Kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili hufanya usafi muda wote kwenye uwanja huo mtakatifu.

Rais wa kitengo hicho Sayyid Naafii Mussawi amesema “Watumishi wa idara ya usafi hufanya kazi muda wote ya kusafisha uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu”.

Akaongeza kuwa “Kazi ya usafi inahusisha kupiga deki, kusafisha mahodhi ya maji, sehemu za kuswalia, kuongoza matembezi ya mazuwaru na kuelekeza sehemu wanazotakiwa kupita mazuwaru, sambamba na kuweka mtandao wa kutoa maji ya mvua”.

Unapofika msimu wa masika kazi huongezeka, hasa mvua inaponyesha. Akafafanua kuwa “Watumishi wetu hufanya kazi ya kutoa maji ya mvua haraka mara tu baada ya mvua kukatika, hali kadhalika idara zingine zote hufanya kazi kwa ushirikiano”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: