Katika mradi wa Arshu-Tilawa.. Majmaa-Ilmi imepokea wageni kutoka mkoa wa Dhiqaar

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imepokea wageni kutoka shule za Qur’ani za wilaya ya Rafai katika mkoa wa Dhiqaar, wamekuja kushiriki kwenye hafla ya Arshu-Tilawa unaofanywa ndani ya ukumbi wa haram ya Abbasi.

Hafla ilikua na mazingira tulivu ya kiroho na imehudhuriwa na mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s).

Msomaji wa Atabatu Abbasiyya bwana Ammaar Alhilliy na Majidu Budairi na msomaji wa mradi wa kiongozi wa wasomaji Abdullah Qassim wameshiriki katika usomaji wa Qur’ani kwenye hafla hiyo.

Ugeni huo umepongeza kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa-Ilmi kwa kufanya miradi tofauti ya Qur’ani tukufu, ukiwemo mradi wa Arshu-Tilawa unaofanywa ndani ya uwanja wa Nuru-Abbasi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: