Kituo cha afya Ummul-Banina chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kinatoa huduma za afya kwa watoto yatima kutoka mkoa wa Misaan.
Mkuu wa kituo Sayyid Ali Bahadeli amesema “Kituo cha afya Ummul-Banina, kinatoa huduma za afya kwa watoto yatima waliokuja kutoka mkoa wa Misaan”, akabainisha kuwa “Kituo kinatoa huduma maalum kwa watoto yatima wenye umri wa miaka (6 – 12)”.
Akasema “Kituo kinahudumia kwa siku hadi watoto 20, kisha hufanyiwa ukaguzi kila baada ya miezi sita” akasisitiza kuwa “Huduma zote zinatolewa chini ya ufadhili wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ikiwa ni pamoja na usafiri, matibabu, malazi, chakula sambamba na kuwapa zawadi mbalimbali”.
Afisa uhusiano wa kituo Sayyid Muhammad Fadhili Abbasi amesema “Atabatu Abbasiyya tukufu ilituma gari maalum katika mkoa wa Misaan, kubeba watoto yatima na kuwaleta katika mkoa wa Karbala kwa ajili ya kufanyiwa matibabu”, akaongeza kuwa “Ratiba waliyopangiwa ilikua pia na safari za mapumziko pamoja na kutembelea malalo takatifu”.