Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imehitimisha ratiba ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa mradi wa kuhifadhi Qur’ani katika mji wa Karbala. Ratiba hiyo ilisimamiwa na Maahadi ya Qur’ani chini ya Majmaa.
Hafla ya kuhitimisha imefunguliwa kwa Qur’ani iliyosomwa na mmoja wa wanafunzi wa mradi, ikafuatiwa na ujumbe wa rais wa Majmaa-Ilmi Dokta Mushtaqu Ali.
Akasisitiza katika ujumbe wake “Kuendelea na kudumu katika kusoma Qur’ani na kuhifadhi, kuzingatia maelekezo ya walimu na kufanyia kazi mafundisho ya Qur’ani kwa kauli na vitendo”.
Washiriki wa program hii walikua wanafunzi (40) na imedumu kwa muda wa miezi mitatu, wamesoma mambo mengi kuhusu namna ya kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, walikua na zamu mbili za masomo kila siku, zamu ya asubuhi na jioni.
Kwa mujibu wa maelezo ya Dokta Mushtaqu “Ratiba ilipambwa na safari za Kwenda kutembelea malalo takatifu na Maraajii Dini watukufu katika mji wa Najafu, zawadi zikatolewa kwa wanafunzi waliofanya vizuri, sambamba na uhamasishaji endelevu unaofanywa na Maahadi kwa wanafunzi wa mradi huu hapa Karbala na mikoa mingine”.