Shindano hilo linasimamiwa na Maahadi ya turathi za mitume na tafiti za kihauza chini ya kitengo.
Shindano linahusu vitabu vitatu vilivyo andikwa na Sayyid Alhakiim, ambavyo ni:
- 1- Khatamu-Nnabiyyina.
- 2- Usulul-Aqidah.
- 3- Faajiatu-Twafu.
Washindi wanne wa kwanza watapewa zawadi zifuatazo:
- 1- Mshindi wa kwanza: Atapelekwa kufanya Umra.
- 2- Mshindi wa pili: Atapelekwa kufanya ziara kwa Imamu Ridhaa (a.s).
- 3- Mshindi wa tatu: Atapewa kompyuta yenye thamani ya (dola 400).
- 4- Mshindi wa nne: Atapewa riyali laki moja na vitabu vya Maahadi.
Shindao litadumu kwa muda wa miezi mitatu, kuanzia mwezi wa Rabiul-Aakhar, matokeo yatatangazwa mwezi kumi na tano Shabani mwaka huu wa 1444h.