Atabatu Abbasiyya tukufu mchana wa leo siku ya Jumanne, imeshuhudia gwaride la wahitimu wapya wa jeshi la majini la Iraq.
Katika gwaride hilo wahitimu wametoa kiapo cha utii mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), umekua utamaduni wa vikosi vingi vya jeshi la Iraq kuja kutoa kiapo cha utii mahala hapa patakatifu.
Na maelfu ya wahitimu wa vyuo vikuu vya taaluma tofauti huja kula viapo vya utiifu katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.