Idara ya wahadhiri wa kike wa Husseiniyya inatoa semina katika sekta ya ulinzi wa taarifa za kwenye kompyuta

Idara ya wahadhiri wa kike Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya, inatoa semina ya ulinzi wa taarifa za kwenye kopyuta (amnu sibrani) kwa baadhi ya mubalighina wa idara hiyo.

Kiongozi wa idara bibi Tamimi amesema kuwa “Hakika hii ni miongoni mwa semina za muwajengea uwezo mubalighina”.

Akaongeza kuwa “Mkufunzi wa semina alikua ni Ustadh Mustwafa Mahmudu Shaakir kutoka kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akabainisha kuwa “Semina imejikita katika mambo mbalimbali muhimu yanayo husu ulinzi wa program za kwenye kompyuta, ikiwa ni pamoja na maana ya neno (Amnu Sibrani) na aina zake pamoja na matumizi ya uhandisi”, akasema kuwa “Kulikua na mihadhara ya kielimu na kiutendaji baina ya mkufunzi na wanafunzi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: