Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake inafanya hafla ya kuhitimu kwa kundi la mwisho la wanafunzi wa masomo ya Qur’ani

Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya imefanya hafla ya kuhitimu makundi mawili ya wanafunzi wa masomo ya Qur’ani.

Kiongozi wa Maahadi hiyo Ustadhat Manaar Aljaburi amesema “Leo tunafanya hafla ya kupongeza wahitimu (26) baada ya kukaa miaka minne mfululizo darasani, ambapo wamefundishwa: kanuni za usomaji wa Qur’ani, nahau, maarifa ya Qur’ani, tafsiri, mantiki, fiqhi, aqida na maarifa ya hadithi”.

Akaongeza kuwa “Hafla imepambwa na usomaji wa mihtasari ya tafiti zilizoshinda kwenye shindano la (ili watafakari aya zake), lililofanywa na Maahadi, ambapo miongoni mwa wahitimu walishiriki na kushinda, nao ni Hamida Daakhil Shaakir, Mirafat Jabbaar na Hina Abdurahim, kisha wahitimu wakapewa zawadi na vyeti”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: