Wanafunzi wa shule za Al-Ameed za wavulana chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wametembelea taasisi ya Waarithu ya kutibu maradhi ya saratani.
Mkuu wa msafara huo Dokta Muslim Alghanimi amesema “Ziara yetu ya leo kwenye taasisi ya kutibu maradhi ya saratani, inalenga kuwapa moyo wagonjwa watoto na kuwapa salamu za siku ya kimataifa ya watoto”.
Akaongeza kuwa “Wanafunzi wetu wametoa zawadi kwa wagonjwa ili kuwatia furaha na kuwapa matumaini ya uhai wao, wakamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awape afya na kuwaponya haraka Insha-Allah”.