Kitengo cha maarifa kinashiriki kwenye maonyesho ya vitabu yanayofanyika katika chuo kikuu cha Al-Ameed kikiwa na zaidi ya aina mia moja za vitabu

Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeshiriki kwenye maonyesho ya vitabu yanayo simamiwa na chuo kikuu cha Al-Ameed.

Maonyesho hayo yanafanywa pembezoni mwa tamasha la (siku ya chuo), katika maadhimisho ya tano toka kuanzishwa matawi 60, na yataendelea kwa muda wa wiki nzima.

Tawi limeshiriki likiwa na aina tofauti za vitabu kutoka kwenye machapisho yake, aidha upangiliaji wa maonyesho hayo unavutia.

Ushiriki huu ni sehemu ya ufikishaji wa machapisho yetu katika jamii na kuongeza wigo wa wanufaika.

Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kinatilia umuhimu uhuishaji wa turathi za kiislamu kwa kufanya uhakiki na kuandika, kimesha andika zaidi ya vitabu miambili vya ukubwa tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: