Majmaa-Ilmi inatoa mhadhara wa kwanza kuhusu (Njia za ufundishaji na mbinu zake)

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imeanza kutoa mhadhara wa kwanza kuhusu (njia za ufundishaji na mbinu zake) kupitia mradi wa Qur’ani Alkafeel.

Mradi huo unasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani chini ya Mjmaa.

Mkufunzi ni Dokta Haidari Shalaa mwalimu wa njia za ufundishaji na lugha ya kiarabu katika chuo kikuu cha Baabil, mihadhara inatolewa kila siku ya Alkhamisi ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Miongoni mwa mada zinazo fundishwa ni, kusimama na kuanza, maarifa ya Qur’ani na njia za ufundishaji, wakufunzi ni walimu bobezi wenye uzowefu mkubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: