Majmaa-Ilmi imepokea wasomi wa Qur’ani kutoka mkoa wa Muthanna

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imepokea wasomi wa Qur’ani kutoka mkoa wa Muthanna, kupitia ratiba ya usomaji wa Qur’ani wa kila wiki katika mradi wa “Arshu-Tilawah”.

Hafla ya usomaji wa Qur’ani ilikua na mazingira mazuri kiroho, kwa baraka ya Qur’ani na utukufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na imehudhuriwa na mazuwaru wengi.

Miongoni mwa waliosoma katika hafla hiyo ni, msomaji wa Atabatu Abbasiyya Fasal Matwaru, Muhammad Zalifu na msomaji wa mradi wa kiongozi wa wasomaji Abbasi Fadhili, Sajjaad Hussein na muongozaji wa hafla alikua ni Hasanaini Jazaairi.

Wageni wameshukuru mapokezi mazuri waliyopewa na wasimamizi wa hafla ya Arshu-Tilawah, wakawatakia mafanikio mema katika kufanya miradi ya Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: