Muwakilishi wa umoja wa mataifa amesema: Tunapongeza miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya kibinaadamu kwa kusaidia makundi ya wanyonge

Muwakilishi wa umoja wa mataifa katika sekta ya wakimbizi nchini Iraq bwana Joo Nikolasi, amepongeza miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kusaidia makundi ya wanyonge katika jamii, hususan waathirika wa matukio ya kigaidi.

Nikolasi katika ziara yake na wajumbe aliofuatana nao kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) amesema “Umoja wa mataifa unathamini kazi kubwa inayofanywa na miradi ya Atabatu Abbasiyya, hasa miradi inayolenga makundi ya wanyonge na watu dhaifu katika jamii”.

Kiongozi wa umoja wa mataifa akasifu miradi na misaana inayotolewa na Ataba, aidha akatoa shukrani kwa mapokezi mazuri aliyopewa na viongozi wa Ataba tukufu.

Ugeni huo wa kimataifa umetembelea baadhi ya miradi ya Ataba tukufu ikiwa ni pamoja na makumbusho ya Alkafeel, akaonyesha kufurahishwa na malikale adimu zilizopo katika makumbusho hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: