Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu imeshiriki kwenye maonyesho ya vitabu katika chuo kikuu cha Al-Ameed

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imeshiriki kwenye maonyesho ya vitabu katika chuo kikuu cha Al-Ameed.

Ugeni kutoka Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa-Ilmi, umehudhuria tamasha la kuadhimisha mwaka wa tano tangu kuanzishwa kwa chuo hicho.

Maahadi imeshiriki kwa kuonyesha machapisho yake na baadhi ya vitambu inavyo fanyia uhakiki, aidha imeonyesha vipeperushi vinavyo tambulisha miradi ya Maahadi ya Qur’ani inayolenga makundi tofauti ya jamii, sambamba na kuonyesha picha za baadhi ya harakati zinazofanywa ndani ya mwaka mzima, kama vile nadwa, makongamano na nyinginezo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: