Miongoni mwa program za kuwajengea uwezo watumishi wapya.. kitengo cha uboreshaji kinafanya warsha ya mtumishi bora

Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinafanya warsha kwa anuani isemayo “Mtumishi bora” katika program ya kuwajengea uwezo watumishi wapya.

Mkufunzi wa warsha Ustadh Ali Hasuun Shimri amesema “Katika warsha hii yamefundishwa mambo muhimu yanayoweza kumsaidia mtumishi kutekeleza wajibu wake kwa usahihi, na vitu muhimu vinavyo msaidia kuboresha uhusiano wake na idara pamoja na watumishi wenzake, sambamba na kuboresha taaluma yake”.

Akaongeza kuwa, “Warsha ilikuwa na mada tofauti, ikiwa ni pamoja na mbinu za kufanya kazi kwa usahihi, kuboresha taaluma, kuboresha uhusiano na watumishi wengine na kujiepusha na hasara kazini”.

Warsha imedumu kwa muda wa saa tatu, wamefundishwa na kufanya mazowezi ya nadhariyya na vitendo, aidha washiriki wametoa maoni yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: