Kuonyesha baadhi ya mali-kale.. makumbusho ya Alkafeel inashiriki katika maonyesho ya chuo kikuu cha Al-Ameed

Makumbusho ya Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya imeshiriki kwenye maonyesho ya chuo kikuu cha Al-Ameed kwa kuonyesha mali-kale za thamani.

Makumbusho imeshiriki ikiwa na idara mbili, idara ya stoo na maabara katika program ya siku ya Ijumaa, kwenye maadhimisho ya mwaka wa tano toka kuanzishwa kwake, idara zimekuja na mali-kale za thamani, ikiwa na baadhi ya miswala.

Makamo rais wa chuo kikuu cha Al-Ameed Dokta Alaa Mussawi alipotembelea maonyesho hayo amesema “Tumeshuhudia picha nzuri inayoakisi umuhimu wake katika kuwa na turathi mbalimbali za kiislamu”.

Hakika kazi hii inafaida kubwa sana ya kushikamana na urithi huu mkubwa na kuendeleza vijana wa chuo kwa kunufaika na historia tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: