Kituo cha utamaduni wa familia kinatoa mhadhara katika chuo kikuu cha Karbala

Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kinatoa muhadhara kwenye kitivo cha uhandisi katika chuo kikuu cha Karbala.

Mhadhiri kutoka kituo hicho Dokta Shimaa Nasoro amesema kuwa “Tumetoa mhadhara wenye anuani isemayo (Hatua za kuelekea kwenye mafanikio) kwa kushirikiana na idara ya maelekezo ya kidini ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya kwa wanafunzi wa kitivo cha uhandisi katika chuo kikuu cha Karbala”.

Chuo kinafanya juhudi kubwa ya kujenga ushirikiano na taasisi za elimu na malezi kwa ajili ya kutengeneza jamii bora ya wanawake yenye kuwatambua Ahlulbait (a.s).

Kiongozi wa idara ya kuwezesha mwanamke katika kitivo cha uhandisi Dokta Nadiya Mussawi ameishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kutoa wahadhiri wenye weledi mkubwa wa kuwajenga wanafunzi na kuwawezesha kupambana katika vita ya vyombo vya habari vinavyo potosha ukweli kuhusu wajibu wa familia na jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: