Kutoka Baabil.. Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu imepokea wageni wa chuo

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imepokea ugeni wa wanafunzi na walimu wao kutoka chuo kikuu cha Baabil.

Wamefanya ziara hii kwa ajili ya kutambua harakati za Majmaa na mipango ya baadae, ziara imepambwa na mihadhara kuhusu utukufu wa Qur’ani na miujiza yake, pamoja na kufanya shindano la Qur’ani.

Kisha wakatembelea kituo cha miradi ya Qur’ani na kuwatambulisha ratiba ya kituo na miradi ya Qur’ani, mwisho wakafanya kikao cha usomaji wa Qur’ani, ambapo wanafunzi wa mradi wa wasomaji wa kitaifa wameshiriki kwenye usomaji Pamoja na ushiriki wa mwimbaji wa kaswida bwana Muhammad Baaqir Qahtwani kwa kusoma kaswida za Husseiniyya.

Majmaa imewapa makazi wageni hao, mwisho wa ziara wamefanya shindano la mpira wa miguu kwa lengo la kujenga ushirikiano baina ya wanafunzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: