Katika maadhimisho ya tano toka kuanzishwa kwake.. Chuo kikuu cha Al-Ameed kinafanya warsha za kielimu

Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya Atabatu Abbasiyya, kimefanya warsha tofauti za kielimu katika wiki ya kuadhimisha mwaka wa tano toka kuanzishwa kwake.

Warsha imeshuhudia utoaji huduma bora za afya, famasiyya, tiba ya meno, uuguzi, aidha walimu kutoka vyuo vikuu vya Iraq wameshiriki katika sekta za kielimu.

Katika moja ya warsha umefanywa mjadala kuhusu uwezekano wa kuchangia uboreshaji wa vyuo vikuu vya Iraq kielimu, jambo hilo linasekta nyingi, kama vile sekta ya viwanda vya nguo, sekta ya tiba, viwanda vya dawa, utengenezaji wa gari na mengineyo.

Wiki ya kitamaduni ambayo maadhimisho haya yanafanyika, bidhaa tofauti za Atabatu Abbasiyya zinaonyeshwa sambamba na maonyesho ya idadi kubwa ya vitabu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: