Makumbusho ya Alkafeel inatarajia kushiriki kwenye kongamano ikiwa na idadi kubwa ya tafiti za kielimu

Kamati ya maandalizi ya kongamano la makumbusho ya Alkafeel imesema kuwa, makumbusho ya Alkafeel inatarajia kushiriki ikiwa na idadi kubwa ya tafiti za kielimu kwenye kongamano la mwaka wa nne.

Kamati ya maandalizi ya kongamano litakalo fanywa chini ya anuani isemayo (Makumbusho ni utambulisho wa kitamaduni) kwa usimamizi wa makumbusho ya Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, aidha imepokea mihtasari ya mada zitakazo wasilishwa na wahadhiri kutoka ndani na nje ya Iraq, kongamano hili ni sehemu ya kujenga ushirikiano na taasisi za makumbusho za kitaifa na kimataifa.

Kamati inatarajia kuwa na mada nyingi za kitafiti zitakazo wasilishwa kwenye kongamano hilo.

Kamati imeongeza muda wa kupokea mada hadi tarehe (1
2m) kwa ajili ya kutoa nafasi kubwa kwa watafiti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: