Waziri wa maji amesema: Miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu inasaidia kutatua changamoto ya maji

Waziri wa maji Sayyid Auni Dhiyabu Abdallah amesema kuwa miradi ya Atabatu Abbasiyya imesaidia kupunguza changamoto ya tatizo la maji wakati wa ziara yake katika Ataba tukufu.

Mheshimiwa waziri amekiambia kituo cha Habari kuwa “Miradi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu hususan miradi ya maji ya visima vya kisasa na kilimo cha umwagiliaji, inasaidia kuondoa changamoto ya ukame”.

Akaongeza kuwa “Kunamatokeo mazuri kwenye miradi ya Atabatu Abbasiyya, inasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo la maji na kuongeza kuwango cha uzalishaji”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: