Katika siku ya kwanza.. chuo kikuu cha Alkafeel kinapokea wanafunzi wapya wa kitivo cha famasia

Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimepokea wanafunzi wapya wa kitivo cha famasia katika mwaka mpya wa masomo.

Wamepokewa na mkuu wa chuo Dokta Saadi Mashkuur na kamati ya wakufunzi wa chuo.

Mapokezi yamefunguliwa kwa Qur’ani tukufu kisha ikasomwa surat Faat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukasomwa wimbo wa taifa na wimbo wa Ataba tukufu (Lahnul-Iba).

Mkuu wa chuo akatoa neno la ukaribisho, na maelezo kwa ufupi kuhusu chuo na muda wa masomo kwenye chuo hicho, kisha wanafunzi wakawekwa kwenye makundi na kutembezwa kwenye madarasa na maabara za chuo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: