Katika kuadhimisha mazazi ya bibi Zainabu (a.s) eneo la katikati ya haram mbili tukufu lashuhudia hafla kubwa

Kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya kongamano la usomaji wa mashairi katika kuadhimisha mazazi ya bibi Zainabu (a.s).

Makamo rais wa kitengo Sayyid Kadhim Swalehe amesema “Hafla ya kuadhimisha mazazi ya bibi Zainabu (a.s) imehudhuriwa na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wengi na wasomaji wa tenzi na mashairi walio soma na kuimba kuhusu kumbukumbu hiyo”.

Hafla imepambwa na mambo mengi ya kufurahisha, yanayo onyesha namna wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wanavyo shikamana na mwenendo wao kwa kuhuisha kumbukumbu zao na kuingiza furaha katika moyo wa Imamu wa zama (a.f).

Waumini wamepongezana na kupeana zawadi kutokana na tukio hili tukufu, wamehuisha ahadi ya kushikamana na mwenendo wa bibi Zainabu na Ahlulbait (a.s) sambamba na kuhuisha mambo yao kwa kufurahi kutokana na furaha yao na kuhuzunika kutokana na huzuni zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: