Jumuiyya ya Al-Ameed imekamilisha semina ya namna ya kuendesha mitandao ya kijamii

Jumuiyya ya Al-Ameed imekamilisha semina kuhusu (namna ya kuendesha mitandao ya kijamii), mkufunzi wa semina Sayyid Ali Swabahu Yaasir amesema “Leo tumehitimisha semina ya (namna ya kuendesha mitandao ya kijamii) iliyodumu kwa muda wa siku mbili, siku ya kwanza wamefundishwa kwa nadhariyya na siku ya pili kwa vitendo”.

Akaongeza kuwa “Semina ilikua na mada nyingi, miongoni mwa mada hizo ni umuhimu wa mitandao ya kijamii katika taasisi, utunzaji wa taarifa, kutatua changamoto za mitandao ya kijamii, namna ya kutunza picha na kuweka machapisho ya pdf”.

Akaendelea kusema kuwa “Semina ilikuwa inalenga kuongeza ujuzi wa matumizi ya mitandao, jinsi ya kujikinga na wavamizi wa mitandao na kuimarisha ulinzi kwenye mitandao ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: