Katika kumbukumbu ya mazazi ya Hauraa (a.s) Idara ya wahadhiri tawi la wanawake yawazawadia wasichana wanaofuata mwenendo wake

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya imefanya hafla kubwa ya kuadhimisha mazazi ya bibi Zainabu (a.s).

Kiongozi wa idara bibi Taghridi Tamimi amesema “Bibi Zainabu (a.s) anamchango mkubwa katika vita ya Karbala, alibeba majukumu makubwa” akasisitiza umuhimu wa kufuata mwenendo wake.

Hafla ilikua na vipengele vingi, ikiwa pamoja na kuangalia filamu inayo onyesha harakati za idara, maigizo yaliyopewa jina la (Zainabu katika karne ya 21), aidha hafla hiyo imepambwa na mashindano ya kujibu maswali kuhusu uhai wake (a.s), ambapo asilimua kubwa ya wahudhuriaji wameshiriki.

Hafla imehitimishwa kwa kugawa zawadi kwa wasichana wanaofuata mwenendo wa bibi Zainabu (a.s) na wanaosambaza mafundisho ya babu yake Mtume (s.a.w.w).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: