Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya anakagua mradi wa upanuzi wa eneo linalozunguka haram takatifu

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyau-Dini, amekagua mradi wa upanuzi wa eneo linalozunguka haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Makamo katibu mkuu wa Ataba tukufu Sayyid Ali Swafaar amesema “Tumetembelea miradi ya upanuzi ya eneo linalozunguka Ataba tukufu, ziara hii ni sehemu ya kukagua utekelezaji wa miradi tofauti”.

Akaongeza kuwa “Tumetembelea eneo la mashariki ya Atabatu Abbasiyya, unapojengwa mradi wa uwanja wa Ummul-Banina (a.s), na barabara ya Kibla ya Imamu Abbasi (a.s) pamoja na eneo lililotengwa kwa ajili ya kujenga makumbusho ya Atabatu Abbasiyya, lililopo mwanzoni mwa barabara ya Kibla ya Imamu Abbasi (a.s)”.

Katika ziara hiyo katibu mkuu amefuatana na rais wa kitengo cha usimamizi wa majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya Mhandisi Qassim Mussawi na kiongozi wa kikosi cha kulinda haram mbili takatifu, kwa lengo la kuhamisha vituo vya ukaguzi na kuviweka sehemu mbadala.

Watendaji wa miradi hiyo ni shirika la ujenzi la ardhi tukufu, chini ya usimamizi wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya na ufadhili wa wakfu-shia na wizara ya fedha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: