Kituo cha matangazo Alkafeel: Tunaelekea kusanifu alama maalum za biashara

Kituo cha masoko na matangazo Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza kufanya usanifu wa alama maalum za biashara.

Kiongozi wa kitengo cha uboreshaji katika kituo hicho Sayyid Sefu-Llah Abdulkarim amesema “Tunaelekea kuangalia alama maalum za biashara, kwa kushiriki kwenye kongamano na maonyesho, kisha tunatoa maoni kwa kuzingatia maendeleo ya kisasa”.

Akaongeza kuwa “Tunatumia mifumo maalum wa kufanya upembuzi yakinifu na kuchuja maoni na fikra tofauti na kuwasilisha yale yanayo kubalika kwa wengine”.

Abdulkarim akasisitiza kuwa “Kituo kipo katika hali ya kujiendeleza kila siku, hadi sasa kimepiga hatua kubwa, aidha kituo kinauhusiano mzuri na shirika na kiwanda cha kutengeneza alama za biashara Alqamaru, na kinafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa”.

Kwa mujibu wa maelezo ya Abdulkarim, kituo cha masoko na matangazo Alkafeel: “Kinafanya kazi na vitengo vyote vya Atabatu Abbasiyya tukufu, kinapokea oda zote za uchapaji wa mabango ya aina tofauti na kutengeneza matangazo ya biashara”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: