Makumbusho ya Alkafeel imepokea ugeni wa wanafunzi wa elimu ya juu

Makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imepokea ujumbe wa walimu na wanafunzi wa elimu ya juu kutoka kitengo cha athari katika chuo kikuu cha Bagdad.

Wageni hao wameangalia mali-kale adimu zilizopo kwenye makumbusho hiyo, wakati wa matembezi yao ndani ya ukumbi wa makumbusho yaliyo ongozwa na kiongozi wa ukumbi huo Shekhe Mahmuud Alhairiy.

Kiongozi wa wageni hao mwalimu wa majengo ya kiislamu Dokta Haidari Swabihawi amesema “Kinacho furahisha zaidi katika kila ziara tunayofanya kwenye makumbusho hii ni upya wake na maendeleo ambayo hushuhudiwa kila sehemu ya makumbusho”.

Wageni wamefurahishwa sana na mali-kale adimu ambazo historia yake inarudi nyuma mamia ya miaka, ziara hii ni sehemu ya kujenga ushirikiano kati ya makumbusho na vyuo vikuu vya ndani na nje ya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: